April 4, 2019


Mwanamke mmoja amejifungua mtoto juu ya mti wa mwembe alipokuwa akiyakwepa mafuriko katika eneo la kati nchini Msumbiji yaliyosababishwa na kimbunga Idai.

Mama huyo afahamikaye kwa jina la Amélia alijifungua mtoto wa kike aitwaye Sara, alipokuwa juu ya mti pamoja na mtoto wake wa kiume mwenye umri wa miaka miwili.

Familia yao iliweza kuokolewa siku mbili baadaye na majirani, kufuatia dhoruba ambayo imewauwa watu 700 nchini mwake.

Tukio hili linakuja takribani miongo miwili baada ya mtoto mwengine kuzaliwa katika mazingira kama hayo. Mtoto huyo, Rosita Mabuiango, alizaliwa wakati wa mafuriko yaliyokumba maeneo ya kusini mwa Msumbiji.

“Nilikuwa nyumbani na mwanangu wa kiume mwenye umri wa miaka miwili ambapo ghafla , bila onyo lolote, maji yalipoanza kuingia ndani ya nyumba yetu,” Amélia aliliambia Shirika la Watoto la Umoja wa Mataifa Unicef.

“Sikuwa na njia nyingine ila kukwea mti, nilikuwa peke yangu na mtoto wangu wa kiume,” aliendelea kusema.

Amélia na familia yake kwa sasa wanaishi katika makazi ya muda ya msaada karibu na Dombe, na wanaelezewa kuwa katika afya nzuri.

Rosita Mabuiango, ambaye sasa ana umri wa miaka 19, aligonga vichwa vya habari za kimataifa baada ya yeye na mama yake, Sofia, kuokolewa na helikopta kutoka kwenye mti uliokuwa umezingirwa na maji ya mafuriko.

Rosita Mabuiango pia alizaliwa juu ya mti wakati mafuriko yalipopiga eneo la kusini mwa Mshumbiji mwaka 2000.

Akizungumza na magazeti ya Mail na Guardian nchini humo, Sofia alisema  alikuwa na uchungu “mkali, mkali sana.”

“Nilikuwa najaribu kulia, kupiga mayowe. Wakati mwingine nilifikiri mtoto alikuwa anatoka, lakini wakati mwingine nikafikiri ilikuwa ni kwa sababu ya njaa.  Watu wengi walipoteza kila kitu katika mafuriko, lakini walau nilipata kitu ,” alisema.

Lakini katika mazungumzo na shirika la utangazaji la Uingereza (BBC) Rosita alisema kuwa ahadi za serikali ya Msumbiji za kumlipia masomo, na ahadi ya kumlipia gharama ya safari ya Marekani iliyotolewa na serikali ya Marekani zote hazijatimizwa.

“Masomo yangu yamekuwa wakati wote yakigharamiwa na mama yangu, sijapokea chochote kutoka kwa serikali,” alisema Rosita.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic