NYIKA AREJESHA FOMU YA KUGOMBEA TENA NAFASI ALIYOJIUZULU YANGA
Wakati Yanga ikiwa katika harakati kambambe hivi sasa kuelekea uchaguzi mkuu wa klabu hiyo, jumla ya watu 28 mpaka sasa wamesharudisha fomu za kugombea nafasi mbalimbali za uongozi ndani ya klabu hiyo.
Katika orodha ya majina hayo, jina la aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Utendaji, Mjumbe wa Kamati ya Utendaji na Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili, Hussein Nyika limo katika orodha.
Ikumbukwe Nyika alitangaza kuachia ngazi hiyo huku akiwaomba radhi wanachama na mashabiki wa Yanga kumsamehe kama kuna mabaya aliyafanya kipindi cha uongozi wake.
Orodha iliyotoka katika kuchukua fomu za kugombea uongozi katika uchaguzi wa Yanga inaonekana kuna watu/waliochukua fomu baadhi yao hata uhalali wa uanachama/upenzi wao katika klabu ya Yanga una ulakini.... walakini....mfano sijui kama Dk Mshindo Msola na Fredrerick Mwakalebela ni Yanga. Pia kuna waliochukua fomu ambao walishashindwa kuongoza taasisi mbalimbali za serikali au michezo huko nyuma na kukumbwa na kashfa mbalimbali zikiwemo Ubadhirifu wa pesa, kutoa ama kupokea rushwa lakini nao pia wamejitokeza....wanachama wa Yanga wanatakiwa kuwa makini mno....kuchuja mamluki na wale ambao hawana maslahi na klabu na maendeleo ya mpira wa miguu nchini....Viongozi wanaotakiwa ni wale ambao ni waadilifu na walio na vision na ubunifu katika katika kuitoa klabu hapo ilipo na kuipeleka katika level ya juu ya maendeleo kulingana na ukubwa wa klabu ulivyo....na kuifanya ijitegemee...wanachama lazima watambue walipotoka wapi walipo na wapi wanataka kwenda....historia yao ya uanachama wa Yanga, historia ya mgombea mmoja mmoja lazima iainishwe na iwekwe wazi ushiriki wake huko nyuma katika kuisaidia klabu kimawazo, fedha na hali yoyote ile...ili wapimwe uwezo wao kabla ya kupewa madaraka!
ReplyDeleteNakupongeza sana kwa hoja zako za msingi,ni Hakika ni muda mzuri(golden chance)kwa wanaYanga kuchagua kiongozi makini mwenye machungu na timu sio wapiga pesa, hao wagombea wanatakiwa waonyeshe ni jinsi gani wako karibu na timu au wamesaidia timu wakati huu Wa matatizo na wana mipango gani na timu sio wajisogezesogeze tu kwenye masuala ya uchaguzi ili wakapige pesa.
ReplyDeleteUko vzr mdau, tunahitaji viongozi makini wenye focus sio wapiga pesa tu,kwanza hao wagombea Wa hizo nafasi waeleze kwa ufupi in namna gani wameisaidia yanga ktk kipindi hiki cha mpito na wana mipango gani na timu? Tuangalie na sura zao in yanga kweli?
ReplyDelete