NYONI: MSIOGOPE, NJOONI TAIFA TUWAUE MAZEMBE
KIRAKA wa Simba, Erasto Nyoni amesisitiza kwa mdomo wake kwamba leo ni lazima washinde mbele ya TP Mazembe hivyo mashabiki wasiogope kwenda Uwanja wa Taifa.
Huo unatarajiwa kuwa mchezo wake wa pili wa michuano hiyo mikubwa Afrika tangu arejee uwanjani akitoka kwenye majeraha ya goti.
Nyoni alisema maandalizi waliyoyafanya wakiwa kambini mkoani Morogoro, hawana hofu ya mchezo huo.
Aliongeza kuwa, sapoti ya mashabiki inahitajika katika mchezo huo itakayowaongeza morali ya kupambana uwanjani ili kufanikisha ushindi.
“Tunashukuru sapoti tuliyoipata katika michezo iliyopita ya Ligi ya Mabingwa Afrika ambayo ilitusaidia kupata matokeo mazuri ya ushindi.
“Matokeo hayo tuliyoyapata yalitokana na sapoti kubwa ya mashabiki wa Simba waliojitokeza kwa wingi uwanjani kutusapoti.
“Hivyo, mashabiki tunawaomba wajitokeze tena uwanjani tutakapocheza na Mazembe na niwaambie wasiogope waje uwanjani,” alisema Nyoni
Tutaujaza uwanja na kushangilia mpaka kieleweke na tulale usingizi mnono
ReplyDelete