April 29, 2019

LEO Jumatatu majira ya saa 10:00 jioni Uwanja wa Uhuru, Dar wanaume 22 watakuwa wakimenyana kutafuta pointi tatu muhimu kati ya Azam FC na Yanga mchezo wa ligi kuu.

Mechi hii ya leo jumla ya nyota watano watakosekana kutokana na sababu mbalimbali na itakuwa ya kwanza kwa Azam na Yanga kukutana msimu huu kwenye Ligi Kuu Bara.

Nyota hawa hapa wataikosa mechi ya leo ambapo kwa Azam FC wachezaji watatu watakosa pambano hili la kukata na shoka ambao ni:-

David Mwantika, Abdallah Kheri ambaye ni majeruhi na Aggrey Morris alipewa adhabu na Kamati ya nidhamu ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).

Kwa upande wa Yanga watamkosa beki mkongwe, Kelvin Yondani anayetumikia adhabu ya kufungiwa mechi tatu pamoja na Juma Mahadhi ambaye hayupo fiti kiafya.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic