UONGOZI wa Mtibwa Sugar umesema kuwa kwa sasa hautakuwa na huruma kwa timu itakayokutana nayo zaidi ya kubeba pointi tatu ili kumaliza ikiwa ndani ya tano bora.
Ofisa Habari wa Mtibwa Sugar, Thobias Kifaru akizungumza na Saleh Jembe amesema kuwa wamejipanga kushinda kila mchezo unaofuata kutokana na morali ya wachezaji pamoja na uwezo.
"Tupo vizuri, tuna nguvu na ari imekuwa kubwa hapo kinachofuata ni kuona kila timu tutakayokutana nayo inatuachia pointi zetu tatu tumejipanga.
"Malengo yetu ni kuona tunamaliza tukiwa ndani ya tano bora kwenye msimamo hivyo hatuwezi kuacha kupambana tukiwa uwanjani, hizi ni salamu kwa ndugu zetu Singida United wanatakiwa wajiandae," amesema Kifaru.
Mtibwa Sugar itamenyana na Singida United Uwanja wa Namfua Mei 3 mwaka huu ikiwa nafasi ya nne baada ya kucheza michezo 32 imejikusanyia pointi 48.
0 COMMENTS:
Post a Comment