April 24, 2019


Jumatatu ijayo Yanga watakuwa na kibarua kizito cha kupambania pointi tatu na Azam FC, sasa Kocha wa Yanga, Mkongomani Mwinyi Zahera amesema akiwatandika wapinzani wake hao basi watakuwa na asilimia kubwa ya kuchukua ubingwa wa ligi.

Yanga wenye pointi 74, wakiwa ndiyo vinara wa ligi, watapambana na Azam FC wanaoshika nafasi ya pili katika mechi ambayo itakuwa ngumu kwa pande zote mbili itakayochezwa Uwanja wa Taifa, Dar.

Kocha huyu ambaye ni msaidizi wa timu ya taifa ya DR Congo, ameliambia Championi Jumatano, kuwa mechi hiyo kwa sasa ndiyo ngumu kwao na wamekuwa wakitafuta mbinu za kupata ushindi.

“Hii ni mechi ngumu kwetu, hawa Azam ni timu nzuri na wenye ushindani wa hali ya juu. Tunawatafutia namna bora ya kupata ushindi mbele yao, tunaamini tukishinda tutajiweka katika mazingira mazuri zaidi ya kuchukua ubingwa.

“Kama tukishinda mbele yao, ina maana itakuwa sasa tufungwe mechi nne, ndiyo wao tena watupate, kitu kikubwa kwa sasa tunapanga mbinu ambazo zitatupa pointi mbele yao ili tuwe na nafasi ya ubingwa,” alisema Zahera.

5 COMMENTS:

  1. Hebu fanya hesabu yako ya kuipata ubingqwa kama ifuatavyo halafu tena ujuwe ukweli:- Ikiwa timu yako itafunga michezo yote iliyobakia na Simba iwe hali iyoiyo au hata Simba ifungwe mchezo mmoja na suluhu moja, jee Yanga itakuwa na point ngapi na Simba itakuwa nazo ngapi halafu utujuilishe au ndoo umeshajuwa Wewe utashinda yote na Simba kupoteza yote??? HAHAHAA. Ni tamaa ya fisi.

    ReplyDelete
  2. Ni ngumu sana kwa Yanga kubeba Kombe mbele ya mnyama, nadhani King Zahera ataelewa pindi tu atakapo shushwa hadi nafasi ya pili na hesabu zake za darasa la kwanza ndo zitakaa sawa.

    ReplyDelete
  3. Yaani ni Vita kati ya Yanga vs TFF, Bodi ya Ligi, Waamuzi, Magazeti, Serikali....na maadui wengine.....sasa mechi ya Azam vs Yanga imehamishwa uwanja wa uhuru....YANGA NI IMARA....YANGA IMESIMAMA KIDETE YANGA INAJENGWA NA WANANCHI WASIOYUMBISHWA PAMOJA NA FITINA NA CHUKI LAKINI MWENYEZI YUKO UPANDE WAO........"DAIMA MBELE NYUMA MWIKO"

    ReplyDelete
  4. "Kama tukishinda mbele yao, ina maana itakuwa sasa tufungwe mechi nne, ndiyo wao tena watupate"

    labda haji hali halisi huyo..Ilivyo sasa ili Simba kufiksha mechi 32 na bado azidiwe na Yanga inabidi afungwe mechi nne, na endapo atashinda mitatu basi stappata point 72...

    Simba akifungwa mechi 2, akatoa droo 2 na kushinda 3 bado staliniana na Yanga..
    Zahera anaonekana haji kinachoendelea Simba..Sio rahisi Simba itafungwa vile wakati Yanga wao wanashinda..Na ajue Azam ambar hawaongei wanajua mechi wao kumfunga Yanga mechi mbili za Azam vs Yanga itawasaidia sana ili kupanda juu

    ReplyDelete
  5. Ni bora Zahera arejee shule akafundishwe hesabu za kutoa na kujumlisha

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic