KOCHA wa makipa wa kikosi cha Serengeti Boys, Peter Manyika amesema kuwa kwa mazoezi waliyoyafanya pamoja na maadalizi wana imani kesho wanaibuka na ushindi mbele ya Nigeria.
Hii ni mara ya kwanza kwa Tanzania kuandaa michuano mikubwa Afrika inayohusu mchezo wa mpira na Serengeti ni wenyeji wa mashindano ya Afcon kwa vijana chini ya miaka 17.
Kesho Jumapili watafungua rasmi pazia la michuano ya Afcon kwa vijana kwa kumenyana na timu ya Taifa ya Nigeria Uwanja wa Taifa majira ya saa 8:00 mchana.
Manyika amesema kuwa wachezaji wana morali ya juu kutokana na mafunzo ambayo wamepewa kabla ya michuano ya Afcon.
"Maandalizi yanakwenda sawa na wachezaji wanatambua kwamba wana kazi kubwa moja uwanjani kutafuta matokeo chanya hakuna jambo lingine zaidi ya hilo.
"Kazi ya mashabiki ni kutoa hamasa hivyo tunaamini uwepo wao uwanjani utatupa nguvu ya kupambana na kufanya kile ambacho wanakihitaji hivyo niwaombe mashabiki watupe sapoti kwa kujitokeza uwanjani," amesema Manyika.
0 COMMENTS:
Post a Comment