April 15, 2019



Kocha mkuu wa timu ya taifa ya vijana ya Tanzania chini ya miaka 17 'Serengeti Boys' Oscar Mirambo amesema bado wana nafasi ya kupata matokeo michezo yao inayofuata licha ya kupoteza mchezo wa kwanza.

Serengeti jana ilifungua pazia la michuano hiyo kwa kucheza na Nigeria na kupokea kichapo cha mabao 5-4 mchezo uliochezwa uwanja wa Taifa.

Kocha Mirambo amesema vijana bado wana moto na uwezo upo wa kupata matokeo licha ya kuanza vibaya mchezo wao wa kwanza.



 "Tumeanza vibaya kwenye mchezo wetu wa kwanza ila haimananishi tumefeli bado tuna nafasi ya kupata matokeo na kushinda mechi zetu zinazofuata, muda upo tutajipanga.

"Ushindani ni mkubwa na makosa yapo hivyo kikubwa ambacho tunaamini bado tuna nafasi ya kufanya vizuri na nia ipo na inawezekana hivyo mashabiki watupe sapoti na waendelee kuwa pamoja nasi," amesema Mirambo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic