April 11, 2019


Klabu ya Simba imeambiwa itarajie kupokea kitita cha shilingi za kitanzania milioni 100 kutoka SportPesa endapo itafanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Pesa hizi Simba watazipata endapo tu watafanikiwa kuiondoa TP Mazembe kwenye hatua hiyo Jumamosi ya wiki hii.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Utawala na Udhibiti wa SportPesa, Abbas Tarimba, amesema Simba watapokea mpunga huo kutokana na mkataba wao ambao walisaini nao unavyosema.

Ameeleza kuwa fedha hizo zitatolewa kama motisha ya kuzidi kuwafanya Simba wajitume vizuri zaidi kwenye mashindano hayo.

katika mchezo wa mwisho uliofanyika jijini Dar es Salaam, Simba ililazimishwa suluhu tasa ya 0-0.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic