April 11, 2019


Mkurugenzi wa Bodi ya Ligi, Boniface Wambura, amesema watafanyia kazi viporo vya Simba ambavyo vimezidi kuwa vingi kutokana na ushiriki wao katika mashindano ya kimataifa.

Kauli ya Wambura imekuja kufuatia mjadala ambao unazidi kushika kasi dhidi ya viporo hivyo ambavyo kwa namna moja ama nyingine vinatajwa kupunguza ladha ya ligi.

Kiongozi huyo amesema wataandaa ratiba maalum ya Simba ili wacheze mechi hizo ili kuendana na kalenda ya TFF ilivyopanga kuwa ndani ya mwezi Mei wanataka ligi iwe imemalizika.

Amefunguka kuwa kuna fainali ya Kombe la Shirikisho 'FA' ambalo pia mshindi bado hajapatikana nalo fainali yake inapaswa kucheza.

Moja ya watu waliolalamikia Simba kuwa na viporo vingi mpaka sasa ikiwa na 11, ni Kocha wa Yanga, Mwinyi Zahera ambaye alieleza kama kuna upendeleo fulani unafanyika.

8 COMMENTS:

  1. Zahera hana maana yeyote mwache aende kucheza BOLINGO

    ReplyDelete
  2. Viporo vinajadiliwa na wanaoionea wivu Simba..Hata wao miaka yote walikuwa na viporo..ila walipokuwa wanacheza mechi za kimataifa walikuwa wanaonfolewa mapema!

    ReplyDelete
  3. Yanga hakuwah kufikisha vporo 10 bali vilikuwa v4 na povu la simba kila mtu anakumbuka walivyoamua kugoma hadi yanga wacheze, matokeo yake yanga alicheza ligi kila baada ya saa 48, kina al ahli wamecheza game jana na wikiend kama kawaida wanapga game za klabu bingwa, tff huo mchezo wa kishabik unawaletea lawama, malinz yanga na viporo vyake v4 karia simba na vyake 11, hatar sana

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ni kweli yanga haijawahi kufikisha viporo 10, lakini je imewahi kufika robo fainali?

      Delete
  4. Sijawahi kumwelewa kabisa huyu Wambura Na sijui kwanin bado yupo ple naona Ni jipu lililoiva kabisa

    ReplyDelete
  5. Kuwa na viporo vingi sio uhakika wa kupata Ubingwa, ukifanikiwa kushinda mechi zako zote ukakusanya pointi zko za kustosha hata mtu awe na viporo huna shida. Yanga wamepoteza point ndio maana wanapata wasiwasi lkn viporo vya Simba sio uhakika wa wao kupata ubingwa.

    ReplyDelete
  6. kilamtu acheze mechi zakee, ni kauli ambayo walikuwa wanaitumia sana kabla hawajaanza kupoteza mechi sasa wamebadilika tena, binadam kazii

    ReplyDelete
  7. Kila mtu ashinde mechi zake ilikuwa kauli mbiu ya migongo wazi.Mambo yamebadilika wameanza stori ya ratiba. Wacheni uoga. Atakayeshinda mechi zake na kuwa pointi nyingi ndio bingwa. Hamna namna wala mbeleko. Enzi za Malinzi kutenga mbeleko zimeshapita.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic