April 20, 2019


MECKY Maxime kocha aliyetibua rekodi ya Simba msimu wa 2017/18 mbele ya Rais John Magufuli  kisha ukaziliwa msemo wa 'kutobolewa tundu' leo ameisimamisha Simba, yenye harufu ya kimataifa baada ya kutinga hatua ya robo fainali kibabe.

Mchezo wa leo uliochezwa uwanja wa Kaitaba, Kagera Sugar walianza kwa kasi ya ajabu na kuandika bao la kwanza dakika ya 18 lililopachikwa kiufundi na Kassim Khamis dakika ya 18 akimalizia pasi ya Ramadhan Kapera aliyewaacha mabeki wa Simba wakishangaashangaa ndani ya boksi.

Bao la ushindi lilifungwa dakika ya 41 baada ya Kagera Sugar kuanza kona fupi iliyopachikwa kimiani na Ramadhan Kapera na kumuacha beki wa Simba Zana Coulibary akinyoosha mkono kuashiria ni bao la kuotea ila mwamuzi akaweka kati.

Kipindi cha pili Simba walianza kwa kasi ila ujanja wao ulidhibitiwa na Kagera Sugar licha ya kufanikiwa kupata bao dakika ya 64 kupitia kwa Emanuel Okwi akimalizia pasi ya Clatous Chama.

Matokeo hayo yalidumu mpaka mwisho wa kipindi cha pili na kuifanya Kagera Sugar kuwa imara mbele ya Simba huku Simba wakiwa dhaifu tena mbele ya Kagera Sugar licha ya kuanzisha muziki mnene Kaitaba.

Matokeo haya ya leo yanaifanya Simba kupoteza mchezo wa pili kati ya 24 ambayo wamecheza wakiwa na pointi 60 huku Kagera Sugaar wakipanda kutoka nafasi ya 17 mpaka 13.

3 COMMENTS:

  1. UTASEMA NINI? UKITOA USHAURI UNAJIBIWA MPIRA UNA MATOKEO 3. INAKERA SANA HAMSIKILIZI USHAURI MPAKA INABOA

    ReplyDelete
  2. hatuna namba mbili Coulibali ni mzigo kocha aelewe asilazimishe kumpanga. Angalia kwa Coustal ambao ni wazuri kuliko kagera timu ilipangwa vizuri wapeni vijana wacheze ligi

    ReplyDelete
  3. kumbe huku wengi tunapenda kuisemea yanga inapoboronga, tunaiacha simba yetu ikitapatapa bila ushauri

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic