April 20, 2019


KIKOSI cha Serengeti Boys leo kimefungashiwa virago rasmi kwenye michuano ya Afcon kwa vijana chini ya miaka 17 baada ya kufungwa mabao 4-2 mbele ya Angola uwanja wa Taifa.

Serengeti Boys ambao hawakuwa na mwanzo mzuri kwenye mashindano kwa kuanza vibaya hali iliyofanya wamalize vibaya licha ya ahadi kubwa waliyopewa na mlezi, Reginald Mengi kulamba milioni 20 na gari endapo wangeshinda mechi mbili na kufuzu kushiriki kombe la Dunia kwa vijana mwaka huu nchini Brazil.

Mchezo wa kwanza walipoteza kwa kufungwa mabao 5-4 mbele ya Nigeria na wakajipa matumaini kuibuka na ushindi mbele ya Uganda matumaini yakazimwa kwa kufungwa mabao 3-0.

Leo Angola wameamua kuipotezea ramani Serengeti kwa kuifunga mabao 4- 2 yanayoipa nafasi kufuzu moja kwa moja kombe a Dunia Brazil.

Matokeo ya Nigeria na Uganda yalikuwa hayana faida kwa Serengeti kwani wametoka sare ya kufungana bao 1-1 mchezo uliochezwa uwanja wa Chamazi.

1 COMMENTS:

  1. UTASEMA NINI? UKITOA USHAURI UNAJIBIWA MPIRA UNA MATOKEO 3. INAKERA SANA HAMSIKILIZI USHAURI MPAKA INABOA

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic