KIKOSI cha Simba leo kimekwea pipa kuelekea Congo DR kwa ndege ya kukodi kwa ajili ya mechi yao ya marudio ya Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya robo fainali dhidi ya TP Mazembe ambayo inatarajiwa kuchezwa kesho Jumamosi.
Meneja wa Simba Patrick Rweyemamu amesema safari kutoka Dar hadi Lubumbashi itachua masaa matatu hadi kutia timu Congo.
"Tumejipanga tukifika tutafanya mazoezi ya mwisho kwenye Uwanja ambao tunategema kucheza mechi siku ya Jumamosi ili kujiaanda rasmi.
"Mipango mingine yote inafanywa na uongozi na tayari kuna viongozi walishatangulia kwa ajili ya kuweka mambo sawa," amesema Rweyemamu.
This comment has been removed by the author.
ReplyDeleteSafari njema na kila la kheri Simba.
ReplyDelete