UONGOZI wa Simba umesema kuwa namna bora ya kupata matokeo kesho ni mashabiki kujitokeza kwa wingi uwanjani na kushangilia mwanzo mwisho bila kupumzika kama ilivyo kawaida yao.
Kesho Simba itacheza na TP Mazembe Uwanja wa Taifa mchezo wa hatua ya robo fainali ligi ya Mabingwa Afrika.
Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara amesema kuwa kikosi kipo tayari na kila mchezaji amepewa jukumu lake hivyo kilichobaki ni mashabiki kujitokeza kwa wingi.
"Hakuna namna nyingine uwanja wa Taifa ni lazima tufanye kazi ya ziada na kupambana kupata matokeo, nina imani kila kitu kinawezekana licha ya ugumu wa mechi ila matokeo tunayahitaji.
"Kikubwa kitakachosaidia kutupa ushindi mbali na wachezaji kuwa tayari bado mashabiki wetu ni muhimu hivyo wajitokeze kwa wingi na kutupa sapoti huku tukicheza kibingwa na mabingwa wenzentu TP Mazembe," amesema Manara.

0 COMMENTS:
Post a Comment