April 5, 2019


Na George Mganga

DAR ES SALAAM, Tanzania - Mwekezaji Mkuu wa klabu ya Simba, Mohammed Dewji Mo, amewataka wanachama na mashabiki wa timu hiyo kujtikokeza kwa wingi katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya TP Mazembe.

Simba inaenda kucheza na Mazembe ukiwa ni mchezo wa hatua ya robo fainali ya ligi ya Mabingwa Afrika utakaofanyika majira ya saa 10 kamili za jioni kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Akizungumza na Waandishi wa Habari leo, Mo amesema lengo lao ni kuzidi kusonga mbele kuelekea hatua ijayo hivyo ni vema wakaja kwa wingi Uwanjani.

Aidha, amewataka pia kununua tiketi mapema leo haswa zile za 4000 kwani kuanzia kesho zitakuwa hazipatikani na badala yake zitapatikana zile za juu pekee.

"Nawaomba mashabiki na wanachama wa Simba kesho tuje kwa wingi uwanjani.

"Tunahitaji kutoa hamasa kubwa kwa wachezaji wetu ili kuwadhoofisha wapinzani na tuweze kupata matokeo.

"Lengo letu ni kuzidi kufanya vizuri na kusonga mbele kuelekea hatua inayofuata."

Kuhusu ujenzi wa Uwanja Bunju

Kati hatua nyingine, Mo amesema kuwa suala la ujenzi wa Uwanja wao unafanyika Bunju jijini Dar es Salaam utakamilika mwezi ujao wa tano.

Mo amesema tayari wameshamalizana na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuhusiana na kuchukua nyasi zao bandarini pamoja na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU).

"Tayari tumeshamalizana na TRA pamoja na TAKUKURU.

"Kwa sasa tutaanza ujenzi wa uwanja wetu na ndani ya mwezi wa tano tutakuwa tumeshakamilisha.

"Hivi sasa tunasubiria mvua zikate kama baada ya wiki mbili ujenzi utaanza rasmi".

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic