April 10, 2019


UONGOZI wa Singida United umesema kuwa kwa sasa kila atakayeshuka kwenye Uwanja wa Namfua anapokea kichapo kutokana na mbinu ya kocha Felix Minziro kujibu.

Singida United waliinyoosha Kagera Sugar mchezo wao wa ligi kuu kwa mabao 2-1 hivyo wana imani leo wataendelea na moto wao wa kutafuta ushindi mbele ya KMC majira ya saa 10:00 Jioni.

Ofisa Habari wa Singida United, Cales Katemana amesema kuwa wamejipanga kwa ajili ya mchezo wa leo hesabu zao ni kupata pointi tatu.

"Hakuna cha kuhofia tena, jeshi lipo kamili kumenyana na KMC, kwa mbinu za Minziro na mipango iliyopo pointi tatu zinatuhusu, mashabiki wajitokeze kwa wingi kutupa sapoti" amesema Catemana.

Singida United ipo nafasi ya 12 baada ya kucheza michezo 32 ikiwa imejiwekea pointi 32 kibindoni.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic