April 3, 2019

MWENYEKITI wa Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Malangwe Mchungahela amewataka wanachama wa Yanga kujitokeza kwa wingi kuchukua fomu ili kugombea uongozi ndani ya Yanga.

Mchungahelea amesema kuwa uchaguzi ni muhimu kufanyika na kwa namna yoyote ile safari hii hakuna kitakachoukwamisha uchaguzi huo.

"Uchaguzi wa Yanga ni lazima ufanyike mwaka huu Mei, 5 hivyo wanachama wajitokeze kwa wingi kuchukua fomu," amesema Mchungahela.

Hii hapa ratiba kamili ya nchakato wa uchaguzi Yanga. 

Aprili 2-7 kuchukua fomu

Aprili 9 Kikao cha mchujo kwa wagombea

Aprili 10 kubandikwa kwa majina yaliyopitishwa

Aprili 11-14 Pingamizi kwa wagombea

Aprili 16-18 Kupitia pingamizi na usaili

Aprili 18-23 Sekretariati kusikiliza maamuzi ya kamati ya maadili

Aprili 24-26 Kukata rufaa

Aprili 27-29 kusikiliza rufaa

Aprili 30- Mei 4 Kampeni 


Mei 5 uchaguzi mkuu.

2 COMMENTS:

  1. kuna baadhi ya vyombo vya habari na waandishi wanakusudia au kutafuta kuwahoji baadhi ya watu ili kuzua chokochoko na malumbano ya aidha uchaguzi ni halali kufanyika au la...uchaguzi utafanyika kama ulivyopangwa na majority ya wanayanga, serikali, TFF, BMT, na Bodi ya Udhamini ya Yanga....hakuna na wala hawatakuwapo wa kuleta chokochoko....hakuna watu walioenda au watakaoenda mahakamani kwani watashughulikiwa na mkono wa serikali....nyie msilete mawazo ya kuchochea vurugu....hii ni amri ya mkuu wa nchi hakuna tena kuruhusu migogoro

    ReplyDelete
  2. Nyie waandishi acheni chokochoko mnatafuta baadhi ya wanachama wasio na maslahi na Yanga mnawafanyia mahojiano ili kuleta mtafaruku hizi mbinu chafu zinajulikana na wanaowatumia wanajulikana sasa hivi hamtaweza katiba ya 1968 kwanini itumike wakati uchaguzi zote zilizofanyika huko nyuma hazikutumia katiba hiyo anayoidai huyo Juma Mwambelo.....uchaguzi utafanyika kama ulivyopangwa na majority ya wanayanga, serikali, TFF, BMT, na Bodi ya Udhamini ya Yanga....hakuna na wala hawatakuwapo wa kuleta chokochoko....hakuna watu walioenda au watakaoenda mahakamani kwani watashughulikiwa na mkono wa serikali....nyie msilete mawazo ya kuchochea vurugu....hii ni amri ya mkuu wa nchi hakuna tena kuruhusu migogoro katika klabu kongwe!

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic