April 3, 2019


LEO ligi Kuu Bara iliendelea licha ya mchezo kama kawaida ambapo timu 12 zilikuwa kwenye viwanja tofaauti kumenyana na matokeo yake ni kama ifuatavyo

Tanzania Prisons 2-0 Mwadui FC uwanja wa Sokoine wafungaji kwa upande wa Prisons ni Salum Kimenya dakika ya 35 na Adam Adam dakika 45.

Lipuli FC 2-0 African Lyon uwanja wa Samora wafungaji ni Zawadi Mauya dakika ya 60 na Miraji Athuman dakika ya  90.


 Ruvu Shooting 1-1 Mtibwa Sugar uwanja wa Mabatini wafungangaji kwa upande wa Ruvu Shooting ni Fully Zully dakika ya  23 aliyesawazisha bao la Riphati Khamis wa Mtibwa Sugar aliyetupia dakika ya  7.

Singida United 2-0 Alliance FC wafungaji wakiwa ni  Kennedy Juma dakika ya  29 na Frank Zakaria dakika ya 45, Mchezo huu uliochezwa Uwanja wa Namfua Geofrey Mwashiuya alionyeshwa kadi nyekundu baada ya kumpiga kiwiko Bigirimana Blaise.


Mbao FC 0-1 Biashara United mfungaji wa Biashara ni George Makang’a 45.

 Coastal Union 1-0 Stand United uwanja wa Mkwakwani Tanga mfungaji wa bao ni Raizin Hafidh dakika ya 63.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic