April 8, 2019




KUTOKANA  na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (Caf) kufanya mabadiliko ya waamuzi wa mchezo wa Ligi ya Mabingwa hatua ya robo fainali kati ya TP Mazembe na Simba uongozi wa Simba umeandika barua kwa Caf.

Habari kutoka ndani ya Simba zimeeleza kuwa matarajio yao ni kuweza kupata majibu muda mfupi kabla ya mechi ili kujua sababu za kubadilishiwa waamuzi.

"Tumetuma malalamiko Caf ya kwa kufanya mabadiliko ya waamuzi wa mchezo wa marudiano wa ambao tutacheza Jumamosi, na njia ambayo huwa tunafanya nao mawasiliano ni kupitia barua pepe na wakati mwingine huwa tunatumia njia ya posta,.

"Bado tunapambana na tunajua mchezo wetu utakuwa mgumu ila tupo tayari kwa ajili ya mchezo wetu, mashabiki wazidi kutupa sapoti," aliongeza kueleza mtoa taarifa.

Barua waliyoandikiwa Simba na CAF kubadilishiwa waamuzi huku sababu ikielezwa ni masuala ya kiufundi inaonyesha awali walikuwa wanasimamiwa na waamuzi kutok nchi ya Ethiopia na kuwaweka kutoka Zambia wachezeshe Simba Vs Mazembe ni hii hapa:-



Barua ambayo Simba wameandika kutaka kupata ufafanuzi juu ya suala hili la kubadilishiwa waamuzi ni hii hapa:-
Simba watacheza mchezo wa marudiano na TP Mazembe Jumamosi Aprili 13, Lubumbashi.


4 COMMENTS:

  1. CHA AJABU NINI? MBONA MECHI YA SIMBA VS YANGA MWAMUZI ALIBADILISHWA? TUPAMBANE TU TUONDOE HOFU WALE TUNAWAPIGA KWAO LUBUMBASHI THIS IS SIMBA.

    ReplyDelete
  2. Mlishawapa minoti?,mbona wasiwasi?,5 zinawasubiri

    ReplyDelete
  3. Wakongo wamezungumza mambo mengi ya hovyo kwa Simba na Tanzania kuwa Simba inashinda kwa mbinu chafu kwenye mechi zake ila mchezo wa mpira ni kazi inayofanywa hadharani na ndio maana licha ya mujungu yote hayo kwa Simba CAF wametulia tuli. Kwani Wanaujua ukweli halisi wa mambo. Simba wanachokosa ni uzoefu tu wa mashindano ya Africa ila wakiamua wanaupiga mpira utashangaa.Nadhani hata hao maspai wa CAF waliokuja kuichunguza mechi ya Simba walipocheza na Vita Club waliondoka wakitabasamu jinsi Africa livyojaa madini ya mpira. Mazembe walikuja Daresalaam kuishikisha adabu Simba baada ya Simba kumgonga mdogo wake vita club na ndio yaliyokuwa matarajio ya wakongo wote na wale wajinga wa jangwani wanaotamani Simba kuondolewa kunako klabu bingwa Africa yakwamba Mazembe wangeanza kutoa kichapo kwa Simba kuanzia Daresalaam na kwenda kumalizia kuizika Simba Lubumbashi. Hata vita walifurahia Draw ya Simba na Mazembe kwa matumaini kuwa ndugu zao hao watawalipizia mchungu yao lakini kilichotokea dar kwa Mazembe hadi kushangilia sare inaonesha kuwa Simba sio wa mchezo mchezo na Vita alifungwa na Simba kihalali kabisa hakuna cha kupuliziwa dawa au kunyeshwa maji yenye sumu. Ombi langu hapa kwa wanasimba tusahau ya mechi iliyopita kwani vijana waljitahidi vya kutosha ila unaweza kusema ulikosekana umakini kidogo kwa wachezaji wetu na kubwa zaidi Mazembe walikuwa na bahati siku ile. Mechi ya Simba Mazembe sasa ni kama hakuja chezwa mechi yeyote kati yao kwa kifupi watu na wachezaji wa Simba wazingatie hili Simba haijapoteza kitu katika mechi hii ya Dareslaam kati yake na Mazembe na pressure zaidi ipo kwa Mazembe hivi sasa kuliko Simba. Ila ombi langu kubwa kwa uongozi wa Simba na zaidi kwa architecture mkuu Mohamedi Mo na watanzania na hasa mashabiki wa Simba kama kuna mechi ambayo tunakiwa kutumia nguvu zetu zote kushinda basi ni hii mechi ya Lubumbashi. Najua malengo na matarajio ya Simba klabu bingwa Africa ameshavuka mpaka ila hawa wakongo wametupaka matope sana Simba kuwa ni wazee wa mbinu chafu na hatuna lolote na ili kusafisha taswira yetu Simba kwa maneno haya kijinga kutoka kwa wakongo basi mechi si mechi kwa Simba isipokuwa mechi ya Lubumbashi. Kwangu mimi mechi ya Lubumbashi kwa Simba ni mechi ya kisasi zaidi ili kuithibitishia Africa na Dunia kuwa Simba hainaga mbinu chafu katika kushinda Dar bali ni uwezo wa mpira na kweli uwezo tunao. La msingi ni maandalizi ya mechi hasa ya ndani ya uwanja kwa wachezaji.Na kwakuwa mechi ya Lubumbashi hata ikimalizika kwa sare bado ni faida kwa Simba basi ni matarajio yetu watanzania kuona wanaoiandaa Simba katika mchezo huo watazingatia kuijenga timu katika maeneo ya ulinzi zaidi kwani hapa ndipo kwenye Donda ndugu la Simba hasa kwenye mechi za ugenini. Naweza kusema mechi hii ya robo fainali kwa Simba ni do or die hasa na ni lazima kushinda kuliko hata mechi ya nusu fainali kwenda fainali kwani kutinga nusu fainali kwa Simba watakuwa tayari walishaiongezea nchi nafasi zaidi za ushiriki klabu bingwa Africa na hapana shaka hata rank ya Simba na ya nchi kimpira itapanda na huko ndiko kukua wakati umefika kwa watanzania wa kulazimisha maendeleo badala ya kukubali kushindwa kirahisi mpaka tumefikia kiwango cha kuwazowesha wapinzani wetu kuwa sisi watanzania ni watu wa kupigwa tu na tukishinda huwa sio jitihada zetu bali tumebebwa au mbinu chafu au bahati,lazima tuamke na mechi ya Lubumbashi Simba lazima tukaicheze kama hatutacheza tena mpira maishani mwetu ni mechi ya kujitoa kwa nguvu zetu zote na watakaobeza waache wabeze ila Simba tunahistoria hiyo na uwezo tunao wa kumfanyia Mazembe kwao.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic