April 8, 2019


HERITIER Makambo mshambuliaji wa Yanga amempiga bao mshambuliaji wa Simba, Meddie Kagere kwenye vita ya kufumania nyavu huku kinara akiwa ni Salim Aiyee wa Mwadui FC mwenye mabao 16 kwa sasa.

Makambo amepachika mabao 2 leo na kuifanya Yanga kushinda nje ndani mbele ya African Lyon mchezo uliomalizika kwa Yanga kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 uliochezwa Uwanja wa CCM Kirumba. 

Mchezo wa kwanza uliochezwa Arusha Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Yanga ilishinda kwa bao 1-0.

Kwenye ligi Kagere ana mabao 14 ,huku Makambo akiwa naye akifikisha mabao 14 hali inayofanya vita ya kiatu cha mfungaji bora msimu huu kuzidi kunoga.

1 COMMENTS:

  1. Kumbuka Simba ana viporo kadhaa ili kagere kufikia idadi ya mechi za Makambo.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic