April 11, 2019



MWENENDO mbaya wa Kagera Sugar kwenye michezo ya ligi kuu umemkasirisha Kocha Mkuu, Mecky Maxime na kusema kuwa leo ataitumia Yanga kuwa daraja la kuipandisha kutoka tano mbovu kwa sasa.

Kagera Sugar anashuka Uwanjani akiwa kwenye nafasi ya 17 na kama akipoteza leo atazidi kubaki chini kwenye msimamo kutokana na kucheza michezo 31 na amejikusanyia pointi 36.

Maxime amesema kuwa ni zamu yake kupanda kwenye msimamo wa ligi kutokana na ushindani ulivyo hivyo ana imani akishinda atajitoa nafasi za chini na kupanda juu.

"Hatupo kwenye nafasi nzuri kwa sasa, tutapambana kupata matokeo kwa sasa ili tujiweke sehemu nzuri licha ya mchezo kuwa mgumu tuna nafasi.

"Ukitazama namna ambavyo tumepishana pointi ni rahisi kwa timu kujitoa pale ilipo na kupaa juu ghafla hivyo nimewaambia wachezaji wangu hatuna cha kupoteza lazima tupambane," amesema Maxime. 

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic