April 11, 2019

KOCHA Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera amesema kuwa kikosi chake kipo tayari kwa ajili ya mchezo wa leo dhidi ya Kagera Sugar utakaochezwa Uwanja wa CCM Kirumba licha ya wachezaji wake kuchoka.

Zahera amesema kuwa wachezaji wake wamecheza michezo mingi mfululizo hali inayowafanya wawe kwenye wakati mgumu wa kutafuta matokeo leo mbele ya Kagera Sugar.

"Wachezaji wangu wamechoka kufuatana na kucheza mechi dhidi ya African Lyon, ila nimewapa mazoezi ambayo yamewafanya wawe fiti kwa ajili ya kupambana.

"Najua mechi itakuwa ngumu tena zaidi ya ile ya Lyon kikubwa ni kupambana na wachezaji nimewaandaa ili tupate matokeo tuzidi kuwa bora zaidi," amesema Zahera.

Yanga ni kinara wa ligi kwenye msimamo baada ya kucheza michezo 30 amejikusanyia pointi 71.

4 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic