April 13, 2019


Baadhi ya mashabiki na wanachama wa Yanga wameutaka uongozi wa klabu yao kuachana na mchezaji wake Ibrahim Ajibu ambaye amekuwa nje ya kikosi kwa takribani wiki tatu sasa.

Mwanachama mmoja ambaye hakutaka jina lake litajwe, amesema ifikie wakati Yanga wawe na maamuzi magumu kwa wachezaji ambao hawana nidhamu huku akimtaja Ajibu.

Mwanachama huyo na shabiki kindakindaki wa Yanga, amesema kuwa Ajibu amekuwa akisingiza anaumwa lakini akiamini kuwa jambo hilo si la kweli.

Ameutaka uongozi kuacha kuficha mambo kwani kila siku umekuwa ukieleza kuwa anaumwa na ndiyo maana amekuwa hasafiri na timu kuelekea mikoani kucheza.

"Ni vema viongozi wetu wakatuweka wazi juu ya suala la Ajibu.

"Sioni tatizo kama wakiachana naye maana amekuwa mbabaishaji kwani hajacheza kwa muda mrefu.

"Natawaka viongozi wangu wawe na maamuzi magumu juu yake kwa maslahi mapana ya klabu na timu," alisema Mwanachama huyo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic