April 13, 2019


KUELEKEA mchezo wa marudio wa Simba na TP Mazembe, kikosi cha Simba ni wazi kimejipanga ambapo hadikufikia juzi Alhamisi tayari kikosi cha kwanza kilishajulikana na kilikuwa kikipewa mazoezi maalum.

Simba ilifanya mazoezi hayo juzi kabla ya jana asubuhi kukwea pipa kuelekea DR Congo kwa ajili ya mchezo huo, ambako ndipo kikosi cha kwanza kinachotarajiwa kuanza kuliwekwa wazi.

Katika mazoezi hayo, Kocha Patrick Aussems, alifanya mazoezi ya aina tofauti na kuunda vikosi viwili, kikiwemo kile ambacho kinatarajiwa kuanza huku mshambuliaji Emmanuel Okwi akirejeshwa kikosini baada ya mchezo uliopita kuanzia benchi.

Kocha huyo aliwagawa wachezaji wake katika makundi mawili ambao kundi la kwanza liliundwa na washambuliaji John Bocco, Okwi, viungo ni Jonas Mkude, Clatous Chama, James Kotei, walinzi ni Erasto Nyoni, Juuko Murshid, Mzamiru Yassin, Mohamed Hussein, Zana Coulibaly na kipa Aishi Manula. Kikosi cha pili kiliundwa na Meddie Kagere, Haruna Niyonzima, Said Ndemla, Hassan Dilunga, Yusuph Mlipili, Asante Kwasi, Mohamed Ibrahim, Paul Bukaba, Rashid Juma, Nicholas Gyan na Deogratius Munishi ‘Dida’.

Katika mazoezi hayo, kocha huyo alionekana kudili zaidi na safu ya viungo pamoja na mabeki kwa kuwafanyisha mazoezi zaidi hasa kwa kukaba na kuwaweka katika mafungu viungo wawili, ambao wanakabana na beki mmoja na baadaye waliweza kucheza vikosi, hivyo viwili kisha likaingia zoezi la penalti.

Hata hivyo, baada ya mazoezi, Aussems alifunguka: “Najua tunaenda kukutana na ugumu lakini kila kitu kinawezekana hata iweje ni lazima tukapambane na kupata matokeo.”

Meneja wa Simba, Patrick Rweyemamu, alinukuliwa akisema: “Timu inaondoka kesho (jana) na wachezaji 18 na viongozi wa timu na benchi la ufundi watakuwa saba na ndege ambapo itakuwa na watu 30 wakiwemo wapishi maalum ambao tunakwenda nao.”

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic