April 22, 2019


TAHADHARI!! Kumekua na Taarifa mbalimbali katika mitandao ya kijamii zikiwanukuu wajumbe na hata Mwenyekiti wa Kamati ya Hamasa juu ya michango inayoendelea, kiufupi mpaka Sasa Kamati haijawai kukaa na waandishi ama mwandishi yeyote kutoa tathmini ya michango inayoendelea.

Hivyo Basi zipuuzieni Taarifa ambazo zinasema Kamati imefanikiwa kupata bilioni 2 na kupata wawekezaji.

Ifahamike kua Kazi ya Kamati ni kuratibu na kutafuta fedha kwa ajiri ya Yanga na sio kutafuta wawekezaji Kama ambavyo imekua ikinukuliwa na baadhi ya vyombo vya Habari.

Sisi kwetu Kamati mwekezaji ni mwanayanga na mwananchi mwenye ndio Maana kauli mbiu yetu katika kuchochea michango ni kua Yanga ni timu ya wananchi na wawekezaji ni wananchi mwenyewe.

Tunathamini michango ya wanayanga kuanzia wanaochanga kiasi kidogo mpaka kikubwa. Mpaka Sasa hatujatoa tathmini ya zoezi tunaloendea nalo, hivyo epukeni uzushi unaofanywa ama kwa makusudi ili kukwamisha juhudi za wanayanga kuchanga ama kwa bahati mbaya .

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic