YONDANI AMVURUGA VIBAYA ZAHERA
KITENDO cha beki kisiki wa Yanga, Kelvin Yondani Alhamisi ya wiki hii kutolewa uwanjani kwa kadi nyekundu, kimemvuruga kocha wa timu hiyo, Mwinyi Zahera ambapo sasa analazimika kumuandaa mbadala wake.
Yondani alitolewa uwanjani kwa kadi nyekundu katika mchezo wa Ligi Kuu Bara ambao Yanga iliibuka na ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Kagera Sugar kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini hapa ambapo alimpiga mchezaji wa Kagera Sugar.
Zahera alisema: “Najua nitamkosa Yondani kama mechi tatu hivi na bado timu ina michezo migumu, hivyo katika mapumziko tuliyonayo nitamtengeneza mchezaji atakayecheza nafasi yake ili tuishinde michezo iliyobaki kwenye FA na ligi kuu.
“Lakini pia wakati mwingine waamuzi wanatakiwa kuwa makini, mimi nilikuwa karibu na tukio hilo, nimeona waziwazi kwamba yule mchezaji wa Kagera ndiye alianza kumpiga Yondani na kisha Yondani naye akajibu, nafikiri ndipo mwamuzi akaona lakini kama ni adhabu wote walistahili kupewa.”
kocha wa ajabu kadi inakwenda kwa aliyerudishia
ReplyDeleteMimi nilivyomuelewa ni kama vile Yondani alivyomtemea mate Kwasi basi ilitakiwa Kwasi naye angegeuka amtemee mate Yondani...Huyu kocha ni mshenzi hadI anatia kinyaa na kichefuchefu
ReplyDelete