April 10, 2019


Kocha Mkuu wa ya Yanga, Mwinyi Zahera, amesema haridhishwi na mwenendo wa ratiba pamoja na uendeshaji wa ligi kutokana na klabu ya Simba kubakiwa na viporo 11.

Kocha huyo ameamua kufunguka tena kutokana na mechi nyingi ambazo Simba wamebaki nazo msimu huu wakati timu zingine zikiwa na michezo michache.

Ameeleza kwa kuwataka TFF na Bodi ya Ligi kupanga ratiba kwa umakini bila kuonesha upendeleo wowote kwa timu zingine jambo ambalo kama yeye halifurahii.

Katika ratiba mpaka sasa inaonesha Simba amesaliwa na mechi takribani 16 ili kumaliza ligi msimu huu lakini kuna baadhi zimebakiza mechi 5.

Zahera pia amesema kuna upendeleo kwa namna moja ama nyingine unafanyika kutokana na timu yake kupangiwa mechi nyingi mfululizo ambazo zinafanya wachezaji wake wapatwe na wakati mgumu.

Zahera amedai wingi wa viporo hivyo kwa Simba inaondoa ushindani wa soka kwenye ligi kwa sababu wengine wamebakiza mechi 5, 6, 7, 8 huku Simba wakiwa wamebakiza mechi 16 kumaliza ligi


11 COMMENTS:

  1. Mpumbavu au ana akili zake kutaka kuiona Simba ikiwa ipo tight kiratiba kabla ya kuwavaa ndugu zake.

    ReplyDelete
  2. Inawezekana ww hufuatilii nchi nyingine zenye timu zinazoshiriki Klabu bingwa afrika au shitikisho lakin hawana viporo namna hii. TFF imeoza na inanuka Umkia mkia tu na TFF inatengeneza mazingira ya kuifanya cmba ichukue tena ubingwa na jambo hili liko wazi mpaka kipofu anaona

    ReplyDelete
    Replies
    1. acha kubwabwaja kama tundu la choo,miundombinu ya Tanzania huwezi kufananisha na hizo nchi unazozilinganisha wewe...ikiwa ulaya kwenyewe wanakuwaga na viporo sembuse sisi cha msingi kila mtu ashinde mechi zake sio kuropokrropokr tu kwani wote watacheza michezo sawa hakuna atakayezidi mbwa nyie

      Delete
  3. Yanga walicheza mechi kumi na moja mfululizo zote taifa(nyumbani)
    ni ligi ya nchi gani inaweza kuruhusu timu kucheza hivyo timu zingine zikizunguka. Sasa analalamikia safari zinaumiza wachezaji. Hilo hakuliona kuwa haikuwa sahihi timu moja kupewa upendeleo ulio kithiri. Anacheza na kurudiana na timu zilizo mkiani wakati Azam FC, hapangiwi maana ni timu ngumu yenye ushindani. Mbona hajalalamika hapangiwi kucheza nayo hata mchezo mmoja toka ligi imeanza na iko DAR.

    ReplyDelete
  4. hakuna nchi yoyote duniani inaruhusu viporo 11 semeni ukweli japo ukweli mchungu
    mambo ya ushabiki fanyeni uwanjani lakini mnapozungumzia ratiba na uendeshwaji wa michezo lazima muwe wakweli na nafsi zenu ziwasute pale mnapojaribu kuficha ukweli

    ReplyDelete
  5. Mlisema viporo vitachacha sasa mmeona havichachi mnaanza kulalamikia ratiba, vingechacha utusingesikia maneno haya, tulieni sindano za moto ziwaingie vizuri.

    ReplyDelete
  6. Mlipopangiwa mechi 11 mfululizo nyumbani ilikuwa sawa.Leo imekuwa nongwa.Mechi yenu nä Azam unapigwa kalenda kila siku.
    Mtibwa mlikuwa kuanza nao Morogoro ikabadilishwa kuwa Dar.
    Kuna mwaka mmecheza mechi zote nyumbani na Ndanda ili mutwae ubingwa. Timu zilipolalamika mkasema zinaropoka. Msimu huu kila mtu ashinde mechi zake hamna namna.

    ReplyDelete
  7. Mcenge kweli..najua anatamani simba icheze na ligi Leo halafu kesho kutwa icheze na TP mazembe.Hanna fara kama Hugo duniani

    ReplyDelete
  8. Na ajue hali ilivyo sasa kila timu icheze mechi zake na mwishoni simba itamzidi Yanga zaidi ya point 11

    ReplyDelete
  9. Yeye ndie anayejuwa kila kitu. Kwa Simb hii usitaraji uningwa

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic