April 10, 2019


Tetesi za soka leo Jumatano Barani Ulaya hizi hapa

Rashford kuongeza mkataba mpya United

Mshambuliaji wa Manchester United na England, Marcus Rashford, 21, anakaribia kutia saini mkataba mpya wa thamani ya pauni milioni 78. (Mirror)

United waanza harakati za kumsajili Alderweireld

United inapania kuanzisha mchakato wa usajili wa Toby Alderweireld kwa pauni milioni 25 kutoka Tottenham. Bado haijawasiliana na Spurs kuhusina na kiungo huyo wa miaka. (Sun)

Conte kutimkia Italy

Meneja wa zamni wa Chelsea Antonio Conte, 49, yuko tayari kujiunga na Inter Milan kama meneja wao mpya ikiwa klabu hiyo itamfanya kuwa Kocha anaelipwa kitita kikubwa zaidi katika ligi ya Serie A. (Mail)

Bale afurahia kuendelea kuwepo Madrid

Wakala wa Gareth Bale, amesema kiungo huyo wa kimataifa wa Wales wa miaka 29, anafurahia uwepo wake Real Madrid na kwamba winga huyo hana mpango wa kurudi Uingereza. (Mirror)

Oblack kupewa mkataba mwingine Atletico

Atletico Madrid inaazimia kutoa ofa mpya kwa kipa Jan Oblak. Kipa huyo wa kimataifa wa Slovenia, 26, pia ametajwa kuwa katika orodha Manchester United kuchukua nafasi ya David de Gea. (Marca)

Hazard kubaki Ujerumani

Kiungo wa kati wa Borussia Monchengladbach, Thorgan Hazard, 26, anaazimia kusalia katika ligi kuu ya Ujerumani ya Bundesliga ili apate nafasi ya kujiunga na Borussia Dortmund.

Hata hivyo klabu yake ya sasa ina mpago wa kumuuza kwa Liverpool baada ya klabu hiyo ya ligi kuu ya England kuzidisha ofa ya euro milioni 42 iliyotolewa na Dortmund. (Nieuwsblad - in Dutch)

Herrera aanza kuangalia ofa katika klabu zingine

Kiungo wa kati wa Uhispania Ander Herrera, 29, anaangalia ofa za timu nyingine na bado hajatia saini mkataba mpya Manchester United kwasababu 'hajaafikiana na klabu hiyo. (ABC - in Spanish)

Arsenal na Tottenham zaingia vitani kwa Perisic

Vilabu vya Arsenal na Tottenham vinapania kumsajili kiungo wa kati wa Inter Milan Croatia Ivan Perisic, 30. (Corriere dello Sport, via Sport Witness)

Rodriguez kuhamia Juventus

Kiungo wa kati wa Real Madrid Mcolombia James Rodriguez, 27, anatarajiwa kuhamia Juventus huku Eden Hazard, 28, akisubiriwa kutua katika uwanja wa Bernabeu. (Marca)

Hazard kutosaini tena Chelsea

Hazard hatatia saini Chelsea, hata ikiwa klabu hiyo itaamua kuzinguana na Real. (Telegraph)

Mazungumzo ya Camacho na Liverpool yakwama

Liverpool huenda ikampoteza kiungo wa kati Mreno Rafael Camacho msimu huu baada ya mazungumzo ya mkataba wake kukwama. (Sky Sports)

Zaha kutimkia Crystal Palace

Mshambuliaji wa Ivory Coast Wilfried Zaha, 26, amesema kuwa ataendelea kuichezea Crystal Palace, licha ya tetesi kuibuka kuwa huenda akarejea Manchester United. (Manchester Evening News)

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic