April 5, 2019


Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera, amelalamika kuwa wameibiwa pointi 10 katika Ligi Kuu ya Tanzania Bara.

Kocha huyo amefunguka kwa kusema "Ligi hii sisi tutaicheza nguvu mpaka mwisho tukimaliza tutaangalia hata kama haya mambo yanayotokea.

"Tukimaliza tutaangalia wapi walitufanyia mambo ya hovyo, ligi tutacheza mpaka mechi ya mwisho na tutacheza na hamu yetu ya kuwina kila mechi.

Tukimaliza tutafanya hesabu tutaangalia wapi tulifanyie nani wapi walitufanyia vitu ya hovyo.

"Hapa leo nimeisha angalia karibu pointi kumi wametuibia.

"Mimi naita kutuibia eeh , najua wanatuibia kabisa zipo mechi karibu nne wametuibia mapointi kabisa .

"Mimi najua kabisa mpango unafanyika , sisi hatushindwi uwanjani tunashindwa vile mipango ambayo wanatufanyia, hatuchezi na timu moja tunajua tunacheza na timu nyingi." amesema Zahera.

CHANZO: UFM

19 COMMENTS:

  1. Visingizio vimeanza. Kila timu ishinde mechi zake.

    ReplyDelete
  2. Wataje hao wezi na ueleze lini umeibiwa na vipi ulivoibiwa na kwanini miezi yote ukanyamaza kimya na weww nafsi yako katika mchezo na ndanda ulimsifu refa na ukawalaumu wachezaji wako. Kila siku vituko vipya na timu yako ikianguka na huku ukiwatuhumu kwa wizi bila ya kuwataja. Vituko vituko vituko

    ReplyDelete
  3. Kocha wa hovyo zahera nae akwaibie simba

    ReplyDelete
  4. Kocha wa hovyo zahera nae akwaibie simba

    ReplyDelete
  5. Kesha ona hawezi kuchukuwa ubingwa sasa ni kilele tuu.kacheze Bolingo

    ReplyDelete
  6. Huyu msema hovyo amefikia tamati.Wanayanga tuanze mapema kabla mambo hayajaharibika zaidi.Kila siku anakuja na jipya.Amekuwa na nguvu kuliko klabu.

    ReplyDelete
  7. Huyo musimuondoe mpaka akumalizeni. Mtu wa ajabu kweli

    ReplyDelete
  8. Mkae mkijuwa yanga kocha wenu ndio anangoja mabilioni ya kukijenga upya kikosi kwasababu anataka kukibadilisha kikosi kamili apate ubingwa mwakani jambo ambalo mustahili. Huyo ataimaliza yimu akukimbieni

    ReplyDelete
  9. Mnamlaumu sana Zahera kwa maneno yake ila nadhan huwa hampo makin kutazama mechi. Angalia mechi ya jana, penalt 2 za wazi nje ya ile tuliyokosa refa kababaika kwenye maamuzi. Nenda Mechi ya Coast kule Mkwakwan kama mliangalia. Nadhan ninyi mnavidonda siyo macho maana mngekuwa na macho mngeona vyanzo vya lawama zake

    ReplyDelete
    Replies
    1. safi ndg, ndo maana akawaambia hawa wasioona vzr wakaangalie marudio kwny azam tv kama ule mpira wa mwisho alishka au hakushka, najua umaskin ndo unachangia marefa kuandaa mazngira

      Delete
  10. This comment has been removed by the author.

    ReplyDelete
  11. Tofauti inaonekana dhahiri kuwa waliowekeza kwenye fedha na timu bora matokeo yanaonekana uwanjani....Simba imekuwa mfano kwenye uwekezaji pia Azam (ambaye alianza siku nyingi) na pia mtaji wa ziada wa Simba ni nguvu ya mashabiki....sasa Yanga watakewasitake lazima watafute wawekezaji wa hali ya juu (makampuni kama Subway, Chinese Companies) kumzidi Mo kwakuwa nao pia kama ilivyo Simba wanamtaji wa mashabiki ila sasa hivi hawajitokezi kutokana na kwamba kikosi chao hakivutii hakina wachezaji wenye kiwango cha juu na hata benchi la ufundi sio la kiwango cha juu....mabadiliko ni lazima ili upate support ya fans lazima uwe na kikosi imara

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kuna mambo mengine ni makosa ya makusudi si uwekezaji. Hata ukiwekeza mali za dunia nzima na figisu zikiendelea namna zilivyo hupati matokeo ndugu

      Delete
  12. This comment has been removed by the author.

    ReplyDelete
  13. Mechi ta kwanza Simba ns Yanga.Simbs alinyimwa goli la wazi alilofunga Okwi kwa madai kwamba kaotea wakati mpira ilitoka kwa Shaibu Ninja.
    Kila timu imepata share yake ya uamuzi mbovu .
    Mambo yanapoanza kwenda mrama ndio makaburi yanafukuliwa.Alikuwa wapi kabla?
    Kila timu imepata pointi kwa gemu walizocheza uwanjani.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kabla ya simba kunymwa goli james kotei alishapga mtu ngumi za kutosha mbele ya refa na yule mama kama uliona vzr alimfata kotei akamuomba asirudie

      Delete
  14. Vincent Chifupe alifanya nini kwenye hiyo mechi?
    Cha ajabu Simba akishinda mechi zake atakuwa mbele ya Yanga kwa pointi hizo 10.Au ndio hizo zilizoibiwa?
    Wajinga watakubali kila ujinga huku timu ikishindwa kuhimili mikimimiki ya ligi?
    Pumzi imekata.

    ReplyDelete
  15. Tulisha tabiri, ushindi was ndumba hauwezi maliza ligi nzima. Yanga ilikuwa inashinda dgahir kwa uchawi was huyu mkongomani. Mechi za mzunguko was kwanza zote Yanga ilikuwa haieleweki inashinda vipi. Ilikuwa inazidiwa kila idara, timu pinzani inangonga myamba tu golini kwa Yanga, possession ndo usiseme wakati mwingine mpaka 30% lakini wao shorts on goal ni moja na goli 1 kwa 0, wanapata point 3. Rejea mechi na KMC, Stand n.k.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic