May 28, 2019


Uongozi wa klabu ya Yanga umesema kuwa mchezaji wake Ibrahim Ajibu amekataa kwenda Simba na anataka kusalia na mabingwa hao wa kihistoria.

Kwa mujibu wa Kaimu Katibu Mkuu wa Yanga, Omar Kaya, ameeleza kuwa hakuna ukweli wowote wa mchezaji huyo kutimkia kwa watani zao wa jadi Simba.

Amesema kinachoelezwa hivi sasa mitandaoni ni tetesi tu na wala hazina ukweli wowote kwasababu mchezaji wanaye wao.

Kaya amesema kila mtu ana uhuru wa kuandika jambo lake na hivi sasa mazungumzo ya kuongeza mkataba baina yake Ajibu na klabu yanaendelea.

Ukiachana na Ajibu, Kaya amesema si pekee tu ambaye mkataba wake unaisha bali kuna wengine wengi ambao wapo nao kwenye mikakati ya kuboresha mikabata yao.

6 COMMENTS:

  1. ile ishu ya mazembe imeishia wap kwani

    ReplyDelete
  2. .....Viongozi wa yanga wanajipalia makaa pasipo kujuwa baadae kunakuja kitu gani ???wanataka kuwaaminisha mashabiki wao kuwa Ajib ni wao kumbe kiualisia huyo ni mali ya Mnyama Simba..Kuweni makini msije chapwa viboko

    ReplyDelete
    Replies
    1. nyie mnaowaaminisha bodaboda fc wenzenu kuwa ajibu ni mali ya simba ndo mjiandae na bakora dadadeki.

      Delete
  3. Ajibu atakiwi kuja Simba sc aliondoka kwa nyodo sasa hivi tuna mtaka wa nini? Au ndio kuuza magazeti! Baada ya mechi na Mtibwa sugar kocha Patrick anakabizi ripoti kwa uongozi ni nani ana achwa ni nani anatolewa kwa mkopo na nafasi zipi zitafutiwe wachezaji wa kuongeza! Wachezaji wanaotakiwa sasa ni wakigeni watu wa shughuli na wenye uwezo mkubwa! Ajibu kwa uvivu ule atawezana kweli na kocha Patrick? Acheni kulazimisha habari za uongo eti Ajibu akataa kuja simba! Kwa mapendekezo ya kocha au uongozi ? Simba bado kuanza kufanya usajili ila kwa sasa ina fanya scouting ya wachezaji wazuri na pindi ligi ikiisha subirieni mwone mambo yatakavyokuwa!

    ReplyDelete
  4. Eti Ajibu hataki kwenda Simba yaani anakusudia anataka kubaki yanga bila ya malipo. Hawa jamaa hawajitambui wanasema nini au wanataka nini kwakuwa wameelemewa. Wakowapi hao wawekaji mliowahidi wakuiusuru yanga

    ReplyDelete
  5. Wanajaribu kumnganganiya Ajibu aliyedhamiria kujinasuwa nao. Eti mchezaji wetu halali

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic