May 27, 2019


KAGERA Sugar ya Bukoba imeamua kutumia sera ya Simba iliyotumiwa kwenye michuano ya kimataifa ya Do or Die ili kubaki kwenye Ligi Kuu Bara msimu ujao.

Kagera Sugar kesho itamenyana na Mbao uwanja wa CCM Kirumba majira ya saa 10:00 jioni na zote zinapambana kustoshuka daraja msimu ujao.

Kagera Sugar ipo nafasi ya 17 ikiwa na pointi 43 huku Mbao FC ikiwa nafasi ya 13 ikiwa na pointi zake 44.

Akizungumza na Saleh Jembe, mshambuliaji wa Kagera Sugar, Kassim Khamis amesema kuwa wanajua utakuwa mchezo mgumu ila wamejiandaa kupata matokeo kwa kwenda na sera ya Do or Die.

"Mwendo wetu wa kesho ni Do or Die hakuna kingine kwa kuwa ni mchezo wetu wa mwisho tunapambana ili tusishuke daraja," amesema.

1 COMMENTS:

  1. Tatizo mnakamia kumfunga Simba halafu mnajifanya mlenda kwa timu zingine.Bora mshuke daraja na mpotee kama Toto Africa.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic