KOCHA Mkuu wa kikosi cha Alliance, Malale Hamsini amesema kuwa wanahitaji pointi tatu za Ruvu Shooting kesho.
Akizungumza na Saleh Jembe, Hamsini amesema kuwa wanajua utakuwa ni mchezo mgumu kutokana na ushindani uliopo ila wamejipanga kupata ushindi.
"Tunapambana kupata pointi tatu kama ambavyo tumetoka kufanya kwenye michezo yetu ya nyuma ni mchezo muhimu kwetu na vijana wapo na morali ya kufanya vizuri," amesema.
Alliance ipo nafasi ya 9 inapambana kubaki kwenye 10 bora huku Ruvu Shooting ikiwa nafasi ya 18 inapambana kutoshuka daraja.
0 COMMENTS:
Post a Comment