May 27, 2019


Harry Kane, anatarajiwa kukwea pipa na kikosi chake cha Tottenham siku ya Jumatano kuifuata Liverpool kwa ajili ya mchezo wa fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Mshambuliaji huyo amekuwa kwenye maandalizi ya kikosi kinachojiandaa kuivaa Liverpool kwenye fainali itakayopigwa siku ya Jumamosi alikuwa nje kutokana na kusumbuliw na majeruhi.
Meendeleo ya mshambuliaji huyo yamekuwa yakiridhisha hali inayotoa nafasi kubwa kwake kuweza kuanza kwenye kikosi kitakachoshuka uwanja wa Wanda Metropolitano.
Meneja wa Totthenham, Mauricio Pochettino anahitaji kumpa nafasi mshambuliaji huyo ili kujua kiasi gani amekuwa imara baada ya kupata majeruhi.
"Kumuanzisha yeye ndani ya kikosi ndiyo kitu ambacho ninakifikiria itakuwa ni maamuzi yangu mwenyewe kumuazisha ama kutomuanzisha kwenye mchezo huo ama michezo mingine, itategemea na namna atakayofanya kama tukishinda itakuwa furaha tukipoteza ni mbaya kwetu," amesema.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic