May 10, 2019



Arsenal imejipoza machungu ya kuboronga kwenye EPL kwa kutinga fainali ya Europa League kibabe.

Arsenal imeichapa Valencia kwa mabao 4-2 kwa Hispania na kutengeneza ushindi wa jumla wa 7-3 dhidi ya timu hiyo ya Hispania.

Shujaa wa Arsenal alikuwa ni Pierre-Emerick Aubameyang ambaye  amefunga mabao matatu, hat trick katika mechi hiyo Arsenal wakiwa ugenini. Moja limefungwa na Lacazette.

Wenyeji walionekana wamepania kupindua kabati baada ya kipigo cha mabao 3-1 jijini London lakini ubora wa safu ya ushambulizi ya Arsenal leo ikawa kikwazo kwao kwa kuwa haikuwapa nafasi ya kupumua kutokana na kutikisa nyavu mfululizo.










0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic