May 27, 2019


UONGOZI wa Azam FC umesema kuwa wamejipanga kulipa kisasi mbele ya Yanga kwenye mchezo wao utakaochezwa uwanja wa Taifa.

Azam FC wana kumbukumbu nzuri ya kupoteza mchezo wa kwanza uliochezwa uwanja wa Uhuru kwa kufungwa bao 1-0 na kupoteza pointi tatu muhimu.

Akizungumza na Salehe Jembe, Kocha wa Azam FC, Idd Cheche amesema kuwa makosa waliyoyafanya mchezo wa kwanza wameyafanyia kazi hivyo hivyo wana imani ya kupata matokeo chanya.

"Tulipoteza mchezo wa kwanza itakuwa mbaya tena tukipoteza mchezo wa pili, tumejipanga na tupo tayari kupambana kwa ajili ya kupata matokeo chanya," amesema.

Azam FC ipo nafasi ya tatu ikiwa na pointi zake kibindoni 72 baada ya kucheza michezo 37.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic