May 27, 2019

TIMU ya Tanzania Prisons, kesho itakuwa na kibarua cha kusaka tiketi ya kubaki kwenye ligi kuu ambapo mchezo wake wa mwisho itakuwa dhidi ya Lipuli FC ambao wao hawana presha ya kushuka ligi.

Prisons ya Mbeya ipo nafasi ya 16 ikiwa na pointi 43 imecheza jumla ya michezo 37 kesho inakamilisha kazi yake ikiwa uwanja wa Sokoine.

Akizungumza na Saleh Jembe, beki wa Prisons, Salum Kimenya amesema kuwa watapambana kupata matokeo chanya ili kubaki kwenye ligi msimu ujao.

"Malengo yetu ni kuona tunabaki kwenye ligi msimu ujao hivyo hatuna namna nyingine ya kufanya zaidi ya kupata matokeo chanya," amesema Kimenya.

Lipuli ya Matola ipo nafasi ya 6 imejikusanyia pointi 49 kesho itakamilisha mchezo wake wa mwisho ikiwa ugenini.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic