MSHAMBULIAJI wa kikosi cha Ndanda, Vitalis Mayanga amesema kuwa wamejipanga kupata pointi tatu muhimu mbele ya Mwadui FC mchezo wao utakaochezwa kesho uwanja wa Mwadui Complex.
Akizungumza na Saleh Jembe, Mayanga amesema kuwa hamna namna nyingine watakayofanya kesho zaidi ya kubeba pointi tatu zitakazowaweka sehemu nzuri kwenye ligi.
"Bado tunapambana kwa kuwa ni mchezo wetu wa mwisho lazima tukomae mpaka mwisho, hakuna cha kutuzuia hivyo tupo tayari kwa ajili ya ushindi, mashabiki watupe sapoti, najua utakuwa mchezo mgumu" amesema Mayanga.
Ndanda FC ipo nafasi ya 7 inapambana kubaki kwenye 10 bora huku Mwadui FC iliyo nafasi ya 19 inapambana kutoshuka daraja.
0 COMMENTS:
Post a Comment