May 26, 2019


NAHODHA msaidizi wa Simba, Mohamed Hussein, 'Tshabalala' ambaye ndiye anayeshikilia rekodi ya kuwa beki bora kwa Simba kutokana na kucheza michezo mingi chini ya Kocha Mkuu, Patrick Aussems, amesema kuwa mashabiki wa Simba wanastahili pongezi kwa kuwapa sapoti mwanzo mwisho.

Tshabalala amecheza jumla ya mechi 29 na ni mechi 16 alizocheza hawakuruhusu kufungwa hata bao la kuotea kutokana na umakini wake na kushirikiana na safu yake ya ulinzi amesema kuwa ni jambo la kujivunia kutwaa kombe tena hivyo wajitokeze kwa wingi jumanne uwanja wa Jamhuri.

"Mashabiki wa Simba ni watu muhimu sana wamekuwa bega kwa bega na sisi hivyo ni jambo la kujivunia, imani yetu ni kwamba tutakuwa nao pia mpaka mchezo wetu wa mwisho, kikubwa sapoti tu," amesema Tshabalala.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic