May 25, 2019


KIUNGO tegemeo wa Yanga, Feisal Salum ‘Fei Toto’, amejikabidhi rasmi Azam FC, baada ya kusema klabu hiyo imekuwa ikimwinda kwa muda mrefu na kwamba yupo tayari kutua kama wataafikiana na Yanga wanaommiliki kwa sasa.

Fei Toto alijiunga na Yanga msimu uliopita kwa mkataba wa miaka miwili akitokea Singida United, ambapo tangu atue klabuni hapo, amekuwa ni mmoja wa wachezaji wenye mvuto mkubwa kwa mashabiki wake, hivyo kama ikitokea akachukuliwa na Azam, ataacha simanzi nzito kwao.

Fei Toto alisema ni kweli Azam wamekuwa wakimfuatilia muda mrefu hivyo kwa kuwa msimu huu unaelekea ukingoni, yeye yupo tayari kutua Azam ikiwa watatimiza vigezo na masharti ya uhamisho kutoka Yanga.

“Sina tatizo la kujiunga na Azam maana wamekuwa wakinifuatilia kwa muda mrefu, lakini mbali na hilo mimi kama mchezaji siwezi kuchagua timu ya kuchezea, zaidi naangalia maisha yangu hasa kwa sasa ambapo umri wangu bado ni sahihi kutafuta maisha bora,” alisema.

Championi lilifanikiwa pia kuzungumza na msimamizi wake Mohamed Kombo juu ya sakata la kwenda Azam, ambaye alisema: “Suala la Fei Toto kutakiwa na Azam kwa sasa mimi bado halijanifi kia, ila ninachoweza kusema ni kwamba, tulikuwa tunasubiria ligi iishe ili twende naye nje ya nchi kwa ajili ya majaribio maana ana ofa tatu nchi tofautitofauti za Ulaya ikiwemo Uingereza.”

4 COMMENTS:

  1. Masikini yangu wenye pesa wanajinyakulia wachezaji kutoka Yanga fukara halafu eti Zahera anangoja kukabidhiwa mamilioni kununuwa nyota akiwemo Mkude. Ama yanga kweli wamekuwa na vichekesho vya ajabu anbapo zamani hawakuwa hivo. Simba imewatibua skili

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hapana. Hii inaonesha Yanga ina wachezaji bora wanaojulikana na kupendwa hata na Timu za nje. Ndiyo maaana timu zinaitaji wachezaji wa viwango ktoka Yanga. Sasa kama timu nyingine hazina wachezaji wa viwango timu gani itakuja kununua wachezaji wabovu. Maaana yake hii ni kwamba wachezaji wa Yanga ni super ndo maana timu mbali mbali zinatumia hela kwanunua.

      Delete
  2. ukweli n yanga inawacheza wenye umri ambao timu nyingi wanaona ni faida mfano Horoya wamemuona Makambo, TP Mazembe Ajibu na huyo Fei

    ReplyDelete
  3. Wale wanaotaka kujiunga na Yanga Kwanza wamuulize Fei Toto kwanini anataka kuhamia Azam kabla ya kumaluza miaka miwili waliyukubaliana na hayo mabilioni wanayoyataja kama kweli wanayo kwanini wamemruhusu Makambo kuondoka ni hadaa tupu

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic