May 20, 2019


KAMPALA, Uganda

Na Mwandishi wetu

WAKATI mshambuliaji wa Yanga, Heritier Makambo akisaini miaka mitatu, Horoya AC ya Guinea, Yanga imeibukia jijini hapa kusaka mrithi wake.

Habari ambazo Championi Jumamosi imejiridhisha nazo ni kwamba, Yanga imefanya mazungumzo na wakala wa straika wa Maroons FC ya hapa, Rashid Agau anayesifika kwa kukokota mpira haswa kwenye eneo la hatari.

Championi Jumamosi limeambiwa kwamba Agau ambaye anasifika kwa kupiga miguu yote atatua Yanga mwezi ujao ili Kocha Mwinyi Zahera amuone kwa ukaribu zaidi.

Mchezaji huyo mwenye nguvu za miguu na weusi wa asili, ni miongoni mwa mastaa wenye umri mdogo wanaofanya vizuri kwenye Ligi Kuu ya Uganda ingawa amekosa namba kwenye timu ya Taifa kutokana na ushindani uliopo.

Wachambuzi wa soka jijini hapa, wamekuwa wakimpa Agau nafasi kubwa ya kuvuka mipaka kwa haraka zaidi katika muda mfupi ujao kutokana na kipaji chake na uwezo wake wa kubadilisha matokeo.

Staa huyo wa zamani wa Onduparaka mwenye ndoto za kucheza Ulaya, alijiunga na Maroons msimu huu wa 2018/19 akiwa huru na kusaini mkataba wa miaka mitatu na kama atajiunga na Yanga basi atakuwa ameitumikia Maroons msimu mmoja tu na huenda vijana hao wa Jangwani wakalazimika kuingia mfuko kumpata.

Mpaka sasa, Agau Rashid amefunga mabao saba ya kiufundi na kuwapita mastaa wenzake kama Pius Obuya na Seif Batte ambao kila mmoja ana mabao manne na ni tegemeo kwenye timu hiyo.

Wakala wake ameliambia Championi Jumamosi kwamba, Maroons imetoa baraka zote kwa Agau kujiunga na Yanga kwa ajili ya majaribio na kama atafanikiwa hawana kipingamizi kwani wanataka kumkuza na kujivunia yeye siku zijazo.

Yanga hawakutaka kufafanua jana kuhusiana na mchezaji huyo huku Makamu Mwenyekiti, Fredrick Mwakalebela akisisitiza kwamba ishu za usajili anafanya Mwinyi Zahera ambaye hata hivyo jana muda mwingi simu yake ilikuwa haipokelewi.

Tayari Championi Jumamosi linajua kwamba Yanga inaendelea na mazungumzo na mastaa wengine wa kigeni kutoka Kenya, Zimbabwe, Rwanda na DR Congo.

Zahera amewaambia viongozi kwamba angependelea asilimia kubwa ya mastaa wa kigeni atakaowasajili msimu huu wawe kutoka kwenye nchi zinazozungumza Kifaransa kwani uwajibikaji wao umekuwa wa tofauti sana Afrika.

Kocha huyo mwenye uraia wa Ufaransa, anataka kumaliza usajili wake mkubwa mapema kabla hajaanza majukumu ya DR Congo inayojiandaa na Afcon ya mwezi ujao nchini Misri.

CHANZO: CHAMPIONI

2 COMMENTS:

  1. Hamna kitu hapo hawa hawana uwezo hata wa kuichezea KMC....Yanga ni timu kubwa jamani watu wanachanga pesa ili kusajili majembe siyo maghalasa kama hayo....habari za magazeti ili yauze hakuna ukweli wowote hapo

    ReplyDelete
  2. acheni ujinga nyie umewahi kuona wapi mchezaji mkali wa uhakika akafanya majaribio,hana ukali wowote huyo kama timu ya taifa tu hayupo kwasababu ya ushindani wa namba kwann msisajiri hao waliomzidi mpaka wanaitwa timu ya taifa?ameachwa mbali sana na okwi huyo

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic