May 20, 2019


UONGOZI wa klabu ya Horoya AC ya Guinea ambayo inashiriki Ligi Kuu nchini Guinea umeamua kweli kum'goa mshambuliaji tegemeo wa Yanga, Heritier Makambo Jangwani ambapo imeripotiwa kwamba wiki hii watatua bongo kumalizia hatua za mwisho za usajili.

Imeelezwa kuwa uongozi wa Horoya kupitia kwa Mkurugenzi wa kamati ya ufundi watatia timu makao makuu ya Jangwani iliyopo mitaa ya Kariakoo ili kukamilisha dili la nyota huyo raia wa Congo.

Haya yote yanatokea baada ya siku chache kupita kwa Makambo kusafiri kwenda Guinea pamoja na Kocha Mkuu Mwinyi Zahera kwa ajili ya kufanya vipimo kwa klabu hiyo ambayo imeshaonyesha nia ya kumtumia nyota huyo msimu ujao kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Zahera amesema kuwa bado Makambo hasaini kwenye timu hiyo licha ya picha kusamaa zikionyesha kwamba amesaini muda wa miaka mitatu.

"Hakuna dlil lolote ambalo limefanyika na kama ikitokea fedha zote zitakuwa za Yanga," amesema Zahera. 

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic