May 24, 2019


BAADA ya kufanikiwa kuvunja mkataba na Yanga, aliyekuwa kipa namba moja wa timu hiyo, Beno Kakolanya anaweza asijiunge na Simba ambayo inadaiwa kumhitaji.

Sababu kubwa ni uhakika wa nafasi ya kucheza kutokana na ushindani wa namba ambao anaweza kukumbana nao kutoka kwa makipa wa sasa wa timu hiyo, Aishi Manula pamoja na Deogratius Munishi‘Dida’.

Meneja wa Kakolanya, Seleman Haroub, alisema mpaka sasa kipa huyo ana ofa nyingi kutoka kwa timu mbalimbali ila bado hajaamua ni timu gani ataenda kuitumikia kwa sababu anahitaji kumuona anakwenda kucheza na siyo kukaa benchi.

Kutokana na hali hiyo, Kakolanya atakuwa na wakati mgumu wa kupata nafasi katika kikosi cha kwanza cha Simba kama atajiunga nayo kutokana na ubora wa Manula pamoja na Dida.

“Tangu tulipopata barua ya Kakolanya kuachana na Yanga, kuna baadhi ya timu za hapa nchini zimeonyesha nia ya kumtaka ila bado mazungumzo ya kina na timu hizo hayajafanyika. “Lakini nahitaji kumuona anakwenda katika timu ambayo atakuwa na uhakika wa kucheza na siyo kukaa benchi,” alisema Haroub

3 COMMENTS:

  1. Teach kufikiria vitu vidogovidogo. Simba itawakilisha nchi. Kwa aina na idadi ya michezo watakayocheza, wanahitaji magolikipa wa kiwango cha Manula Mkiwa na magolikipa wote wazuri wote wanacheza kwa kupangiwa mechi zao. Simba waliwahi kuwa na Athumani Mambosasa , Hassan Mlapakolo na wakamuongeza Mahadhi Al Jabrywote ni wa viwango vya kimataifa. Yanga ilikuwa na Elias Michael na Muhidin, wote hatari wa kimataifa. Kakolanya una faida gani kuchezea Ndanda (mano tu) mechi zote 38 za ligi badala ya kuchezea Simba nusu ya mechi hizo (19) lakini Sevilla watakuona na sasa wamealikwa kwenda Spain kwa mechi 5 kule. Fanya maamuzi ya maana, akili za meneja changanya na zako, AMUA.

    ReplyDelete
  2. Tuache kufikiria vitu vidogovidogo. Simba itawakilisha nchi. Kwa aina na idadi ya michezo watakayocheza, wanahitaji magolikipa wa kiwango cha Manula Mkiwa na magolikipa wote wazuri wote wanacheza kwa kupangiwa mechi zao. Simba waliwahi kuwa na Athumani Mambosasa , Hassan Mlapakolo na wakamuongeza Mahadhi Al Jabrywote ni wa viwango vya kimataifa. Yanga ilikuwa na Elias Michael na Muhidin, wote hatari wa kimataifa. Kakolanya una faida gani kuchezea Ndanda (mano tu) mechi zote 38 za ligi badala ya kuchezea Simba nusu ya mechi hizo (19) lakini Sevilla watakuona na sasa wamealikwa kwenda Spain kwa mechi 5 kule. Fanya maamuzi ya maana, akili za meneja changanya na zako, AMUA.

    ReplyDelete
  3. Tuache kufikiria vitu vidogovidogo. Simba itawakilisha nchi. Kwa aina na idadi ya michezo watakayocheza, wanahitaji magolikipa wa kiwango cha Manula Mkiwa na magolikipa wote wazuri wote wanacheza kwa kupangiwa mechi zao. Simba waliwahi kuwa na Athumani Mambosasa , Hassan Mlapakolo na wakamuongeza Mahadhi Al Jabrywote ni wa viwango vya kimataifa. Yanga ilikuwa na Elias Michael na Muhidin, wote hatari wa kimataifa. Kakolanya kuna faida gani kuchezea Ndanda (mfano tu) mechi zote 38 za ligi badala ya kuchezea Simba nusu ya mechi hizo (19) kwa mfano lakini Sevilla watakuona na sasa wamealikwa kwenda Spain kwa mechi 5 kule. Fanya maamuzi ya maana, akili za meneja changanya na zako, AMUA.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic