February 28, 2021


PATRICK Sibomana ameibuka na kudai yupo kwenye mpango wa kuifungulia mashitaka Klabu ya Yanga kwenye Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa), kwa kile alichokieleza kuwa, ukiukwaji wa makubaliano ya malipo ya stahiki zake.

 

Hii inakuja ikiwa ni siku chache baada ya Fifa kuitaka Yanga kumlipa aliyekuwa mshambuliaji wa timu hiyo, Amissi Tambwe.

 

Sibomana ambaye ni mshambuliaji aliichezea Yanga kwa msimu uliopita kabla ya kuachwa mwishoni mwa msimu huo.


Nyota huyo anayeumia zaidi mguu wa kushoto amesema: “Tulikubaliana kwamba Yanga wanilipe fedha zangu za usajili ambazo zilibaki kiasi cha dola 10,000 (Sh mil 23).

 

“Kwa kuwa niliishi nao vizuri na nilijua timu ilikuwa haina fedha, tulipanga wanilipe kwanza fedha ya miezi mitatu pamoja na fedha ya usajili ambayo jumla yake ni dola 16,000 (Sh mil 36.9) ambayo nilikatwa hadi kufikia dola 14,500 (Sh mil 33.4).



“Tukakubaliana kwamba wangenilipa Oktoba 30, mwaka jana ambapo walinipatia dola 3,000 (Sh mil 6.9) ikabaki dola 11,500 (Sh mil 26.5) ambapo niliwaambia wanipatie zote, lakini cha kushangaza walinitumia dola 1,500 (Sh mil 3.4) na mwezi Januari mwaka huu wakanipatia pesa iliyobaki, ambapo deni likabaki dola 4,000 (Sh mil 9.2.

 

“Sasa mimi nilikwazika kwa sababu walikuwa wakinilipa kwa muda wanaotaka na kwa kiwango wanachotaka, kila nikiwatafuta viongozi wamekuwa wakiniambia kwa nini nawaandikia barua mara kwa mara, wakati inawezekana nikarejea kwao siku moja.

 

"Mimi naona wananionea, kwa kutofuata makubaliano tuliyokuwa nayo na sijui kwa nini? Hivyo kwa sasa tayari nimewaandikia barua Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), na kama suala langu litakuwa halijapatiwa ufumbuzi hadi kufikia Machi 1, basi sitakuwa na njia nyingine zaidi ya kupeleka malalamiko yangu Fifa.


“Kiukweli nisingependa kufika huko, lakini nadhani wao ndiyo wananisukuma kufanya hivyo,” amesema Sibomana.

 

Alipotafutwa Kaimu Katibu Mkuu wa Yanga, Haji Mfikirwa azungumzie ishu hiyo alisema: “Taarifa kuhusiana na madai ya Sibomana tunazo hivyo tunashughulikia.".

 

Ulipotafutwa uongozi wa TFF kuthibitisha taarifa hiyo, Ofisa Habari wa TFF, Clifford Ndimbo amesema: “Kwa upande wangu siwezi kusema lolote kwa sasa mpaka pale nitakapopata nafasi ya kuwasiliana na kamati ya sheria kuhusiana na hilo. 

6 COMMENTS:

  1. Mnachafua wenyewe brand ya timu halafu mkitaniwa kidogo tu mnatishia kwenda mahakamani.... Kweli nyie ni utopolo

    ReplyDelete
  2. Usajili wa mbwembwe bila malengo. Sasa walioeni hawa wataendelea kuwaharibia image yenu kimataifa. Akienda na hutu FIFA, itaonekana yanga ni matapeli wazoefu, brand inachafuka jamani.

    ReplyDelete
  3. Brand ipi?Utapeli haujawahi kuwaacha huru Lipeni haku za watu Au hii pia ni njama ya kuvuruga na kukashifu brand yenu
    Hamkosi visingizio lakini uwajibikaji sifuri.

    ReplyDelete
  4. Lazima Yanga iwe Bingwa hata mkileta story za kututoa kwenye focus weka taja na mwingine anayedai tu(hiyo inaitwa Vita ya kutechnologia)

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hizi ni habari za kuungwa kuungwa...kuna watu wanataka kutengenezewa njia

      Delete
  5. dawa ya deni kulipa duuu naamini wapo wengi wanaodai utopolo fc

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic