MENEJA wa Paris Sant-German, Thomas Tuchel amesema hawezi kuwaruhusu wachezaji wake wote wawili, Neymar Jr na Kylian Mbappe kuondoka kwenye kikosi hicho msimu ujao.
Wachezaji wote wawili wamekuwa wakihusihwa kuondoka kikosini hapo msimu ujao kwenda kutafuta changamoto mpya.
Neymar amekuwa akihusishwa kujiunga moja kwa moja na kikosi cha Real Madrid baada ya kujiunga na PSG mwaka 2017 akitokea Barcelona kwa dau la Euro milioni 198.
Meneja wa PSG amesema "Ninahusika kulisimamia hili kwa kiasi kikubwa, kwa sasa tupo mwezi Mei, uongozi unajua utatoa ukweli kuhusu hizi taarifa za hawa kuondoka mwezi ujao.
"Vitu vipo kama vilivyo, kuna mambo mengi sana ambayo yanazungumzwa kwa sasa hii inamaanisha kwamba tupo vizuri na vijana wetu wana vipaji vya kweli, nikiwa ni meneja kwenye timu hii malengo yangu ni kuona wachezaji wote ninabakiwa nao kama ambavyo nilianza nao ndivyo nitakavyomaliza nao, kazi haijaisha," amesema.
0 COMMENTS:
Post a Comment