May 14, 2019


MSHAMBULIAJI wa Simba, Meddie Kagere amesema kuwa watapambana msimu huu kuona wanafanikisha malengo ya timu kutwaa ubingwa.

Kagere ni kinara wa kucheka na nyavu ambapo mpaka sasa ametupia jumla ya mabao 20 kwenye ligi akifuatiwa na mshambuliaji Heritier Makambo wa Yanga na Salum Aiyee wa mwadui wenye mabao 16.

Akizungumza na Saleh Jembe, Kagere amesema kuwa ushindani ni mkubwa na kila timu inapambana kutafuta matokeo.

"Kila timu inapambana kutafuta matokeo, kwa nafasi ambayo tupo bado tunaweza kufanya vizuri na kushinda michezo yetu iliyobaki.

"Mashabiki tunawapenda na sapoti yao inatufanya tuzidi kupambana hivyo tunaamini tutafikia malengo ambayo tumejiwekea kuona namna gani tutatwaa ubingwa," amesema Kagere.

2 COMMENTS:

  1. Urakozi chane wa muhungu we wachu.Komera chane chane

    ReplyDelete
  2. Enter your comment...Bila shaka, ubingwa Msimbazi.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic