BAO la Omary Ramadhani wa KMC dakika ya 61 nje ya 18 akimalizia pasi ya Abdull Hillary limetosha kuifanya KMC kupata pointi zake tatu ugenini kwa mara ya kwanza msimu huu.
Ushindi huo ni kama kisasi kwa KMC, kwani walipocheza na Mbeya City walipoteza kwa kufungwa bao 1-0.
KMC ambayo ipo chini ya kocha mkuu, Etttiene Ndiyaragije imeshinda michezo yake miwili ya hivi karibuni baada ya kuanza kupata ushindi mbele ya Mwadui uwanja wa Uhuru kwa mabao 2-0 na jana ushindi wa bao 1-0.
Kwa sasa KMC inaendelea kujikita nafasi ya sita baada ya kucheza michezo 34 imejikusanyia pointi 45 huku Prisons wakiwa nafasi ya tisa baada ya kucheza michezo 34 wana pointi 42.
Michezo ya mwisho ya KMC ugenini ilikuwa dhidi ya Mbeya City ambapo walipoteza kwa kufungwa bao 1-0 pia ule wa Singida United walitoshana nguvu kwa suluhu ya bila kufungana na mchezo wao uliofuata walifungwa mabao 2-1 na Simba.
0 COMMENTS:
Post a Comment