KOCHA wa Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera amesema kuwa leo atapambana kupata matokeo mbele ya Ruvu Shooting mchezo wa Ligi Kuu Bara.
Yanga ipo nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi endapo itashinda leo itarejea kuwa kinara.
"Najua utakuwa mchezo mgumu ila nipo tayari kwa ajili ya kupata matokeo. wachezaji wangu wapo tayari kupambana nina imani tutafanya vizuri," amesema Zahera.
Yanga imecheza michezo 35 imejikusanyia jumla ya pointi 80 ip nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi huku kinara akiwa ni Simba mwenye pointi 82.
0 COMMENTS:
Post a Comment