May 25, 2019




 ALIYEWAHI kuwa kocha wa Simba, Dylan Kerry ameachiangazi katika klabu yake ya Black Leopards ya Afrika Kusini baada ya kutoridhishwa na mwenendo wa klabu hiyo.
 Inadaiwa kuwa kocha huyo yuko mbioni kujiunga na klabu ya SuperSport United ya nchini humo inayoshiriki Ligi Kuu ya Afrika Kusini.

 Kerr ambaye ni raia wa Uingereza aliwahi kuinoa klabu ya Simba lakini hakufanikiwa kutwaa taji na baadaye alikwenda kujiunga na klabu ya Gor Mahia ya nchini Kenya ambako aliweza kutwaa ubingwa.
 Kocha huyo alijiunga na Black Leopards inayoshiriki Ligi Kuu ya Afrika Kusini mapema  Novemba 2018 na ameachia ngazi  Mei 2019.
 Hata  mwenyekiti wa klabu ya Black Leopards, David Thidiela amethibitisha barua ya kujiuzulu kwa kocha  huyo Kerr ndani ya klabu yake. Kiongozi  huyo amesema kuwa viongozi wa klabu watakapokutana watatangaza taarifa rasmi  ya kujiuzulu kwa kocha huyo.
 Kerr amesema:“Ni kweli naondoka Black Leopard lakini siwezi kusema kwa nini naondoka pale kwa sasa ila jueni tu kuwa nimejiuzulu.
“Nahitaji wakati kwa sasa  mama yangu ni mgonjwa na yupo hospitali ni lazima kwanza  nimshughulikie hivyo kwa sasa nipo England mama yangu ni muhimu zaidi. Nitawajulisha baadae ninaelekea wapi.
 Kocha huyo akiwa na timu hiyo alifanikiwa kuwa kocha bora mara mbili mwezi Desemba na Januari na alisaini mkataba wa miaka mitatu na klabu hiyo.
 Kerr alisimamia jumla ya mechi 21 na katika mechi  hizo alishinda mechi sita na kutoa sare sita huku akipoteza mechi tisa.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic