May 25, 2019


NAHODHA wa Yanga, Ibrahim Ajibu leo amewaaga viongozi wa timu zake zote mbili alizotumikia kabla ya kupata nafasi ya kujiunga na TP Mazembe ya Congo msimu ujao.

Ajibu amesema kuwa amepitia timu nyingi kabla ya kupata nafasi ya kujiunga na TP Mazembe hivyo hana budi kuwashukuru viongozi wote ambao wamemkuza kabla ya kufikia hatua ambayo ameifikia.

"Kwa nafasi ya pekee naishukuru timu ya Simba ambao wamenifanya kufika hapa nilipofika bila kumsahau ofisa habari wao Haji Manara ambaye amekuwa ni mtu wa hamasa kutoa moyo pamoja na kujenga saikolojia ya mchezaji.

"Nimekaa miaka miwili ndani ya Yanga, imekua bora kwangu licha ya changamoto za kimaisha ambazo nimezipitia ila upendo wa mashabiki wa Yanga ni mwingi sana sina cha kusema zaidi ya asante, wakati wote nitawakumbuka," amesema Ajibu.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic