KOCHA mkuu wa Yanga, Mkongomani, Mwinyi Zahera leo amekwea pipa kurejea kwao DR Congo huku akimuachia majukumu ya maandalizi ya mchezo wao dhidi ya Mbeya City msaidizi wake Noel Mwandila.
Kocha huyo ameeleza kuwa amerejea kwao kwa ajili ya masuala binafsi na ya kifamilia na akisema anatarajia kurudi nchini Mei 19 mwaka huu.
Jana Zahera aliongoza kikosi chake kucheza mchezo wake wa 36 mbele ya Ruvu Shooting na waliibuka na ushindi wa bao 1-0 lililopachikwa na Pappy Tshishimbi.
Akizungumza na Saleh Jembe, Zahera amesema kuwa anatarajia kurudi kabla ya mchezo wao dhidi ya Mbeya City hivyo majukumu yote ya maandalizi kamuachia msaidizi wake ashughulike nayo.
“Nimesafiri jamani niko kwenye ndani ya ndege naelekea Congo hivyo majukumu yote nimemuachia kocha msaidizi mimi natarajia kurudi tarehe 19,”alisema Zahera.
0 COMMENTS:
Post a Comment